Godbless Lema: Niko tayari kuuza figo yangu kwaajili ya matibabu ya Tundu Lissu. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 18 November 2017

Godbless Lema: Niko tayari kuuza figo yangu kwaajili ya matibabu ya Tundu Lissu.

Mbunge wa Arusha Mjini Mhe Godbless Lema amesema hata kama gharama za matibabu ya Tundu Lissu yakifika Trilioni moja, watakuwa tayari kuuza figo zao.

Akizungumza jana Novemba 18 katika kata ya Siuyu iliyopo Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Lema amesema utekelezaji wa majukumu ya kisiasa ukiwa upinzani wakati huu ni ngumu kutokana na kuwindwa kila uchao.

Amesema pamoja na ugumu huo hawajarudi nyuma na kisasi cha wasiopenda mabadiliko na wanaochukia kukosolewa kimedhihirika kwa vitendo alivyotendewa Lissu.

"Lissu yupo kitandani risasi mwili mzima, gharama za matibabu yake ni kubwa, lakini hata ikifika trilioni moja na tukawa hatuna fedha tutauza figo zetu kuendelea kugharamia matibabu yake" amesema Lema.

Amesema Lissu amekuwa alama ya haki katika taifa kutokana na kuamua kuwa upande wa haki

No comments:

Post a Comment

Popular