Geita: Mkuu wa mkoa awaweka ndani masaa 48 Afisa Elimu wa Wilaya na mkuu wa shule kwa kukaidi maagizo. - KULUNZI FIKRA

Saturday, 18 November 2017

Geita: Mkuu wa mkoa awaweka ndani masaa 48 Afisa Elimu wa Wilaya na mkuu wa shule kwa kukaidi maagizo.

 
 Mkuu wa mkoa  baada ya kumaliza shughuli katika Kituo cha Afya Mganza, ametembelea Mradi wa pili wa Ujenzi wa Bweni la wanafunzi Shule ya Sekondari Zakia Meghji ambalo linajengwa kwa ufadhili wa pesa za P4R kwa gharama ya Tsh. 75,000,000.00 litakalotakiwa ku-accommodate wanafunzi 80 kwa mujibu Melekezo ya Wizara yenye dhamana juu ya utaratibu wa fedha hizo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 31 Oktoba, 2017  mkuu wa mkoa alipotembelea Ujenzi wa Bweni hilo alibaini ukiukwaji wa taratibu za fedha hizo za P4R, ambapo ujenzi wa Bweni uliofanyika katika Shule hiyo ya Zakia Meghji ulijengwa kwa kuweza kutosheleza wanafunzi 56 badala ya wanafunzi 80.

 Mkuu wa mkoa  alichukua hatua ya kuwaelimisha viongozi na watendaji wa Shule, Halmashauri na Wilaya kwa ujumla juu ya matumizi ya fedha hizo yanavyotakiwa kuzingatiwa, na alidiriki kuthibisha maelekezo hayo kwa kuwasiliana na Wizara husika na wote kwa pamoja waliokuwepo mahali hapo walijiridhisha.

Hivyo, mkuu wa mkoa  aliagiza ujenzi huo usimamishwe na yafanyike marekebisho ya kuonngeza ukubwa wa Bweni hilo kwa maana ya kutosheleza idadi ya wanafunzi 80 badala ya wanafunzi 56 kama walivyojenga sasa.

(Ikumbukwe kuwa wakati huo Bweni hilo lilikuwa halijapauliwa bado). Mkuu wa mkoa  alielekeza Viongozi wenye dhamana na maslahi ya Mradi huo watekeleze maagizo hayo na kusimamia ipasavyo Mradi huo na kuhakikisha thamani ya fedha hiyo inaonekana.

Leo (jana) mkuu wa mkoa  alipotembelea Mahali hapo amekuta ukiukwaji wa Maelekezo aliyoyatoa hivyo amechukua hatua za kisheria kwa kumuagiza Kaimu OCD Chato awapeleke Polisi Afisa Elimu Sekondari Chato pamoja na Mkuu wa Shule ya Sekondari Zakia Meghji kwa muda wa masaa 48 kwa kukiuka Maagizo halali yaliyotolewa na Mamlaka.

Aidha, Mkuu wa mkoa  amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri  awachukulie hatua za kinidhamu kwa watendaji hao kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa Umma.

No comments:

Post a Comment

Popular