Godbless Lema amjibu Lawrence Masha kwa kutoa sababu zisizo na mashiko. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 15 November 2017

Godbless Lema amjibu Lawrence Masha kwa kutoa sababu zisizo na mashiko.

 Baadhi ya wabunge na viongozi wa CHADEMA wametoa maoni yao baada ya mwanachama wao Lawrence Mahsa kujivua uanachama na kujibu tuhuma alizozitoa zikiwa kama sababu za kujivua kwake.

Kwenye kurasa zao mbali mbali za mitandao ya kijamii Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika ujumbe akisema safari ya kupigania usawa na haki ni safari ndefu, kwa yeye mwanaume kushindwa kuhimili safari hiyo ni aibu kwani kuna wananwake ambao bado wanaendelea kuhimili ugumu wa safari.

“Lawrence Masha , struggle ya kupigania usawa,haki na demokrasia, ni safari ndefu na ngumu ,wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na wanawake imara wanaendelea na safari,sio uamuzi mbaya uliochukua ila ni uamuzi wa aibu . Utajua baadaye na sio sasa”, ameandika Mhe Godbless Lema.

Naye Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari ameandika ujumbe wake akisema wanajua sababu za Masha kuondoka CHADEMA na sio zile ambazo amezitaja, na hata hivyo wanaheshimu mamuzi yake.

“Tunaojua sababu za Masha kutoka CHADEMA zile kwenye barua yake tunajua ni danganya toto, tunajua sababu na tunaziheshimu. Kuthibitisha kuwa CHADEMA imejipanga kuingia ikulu, angalia takwimu za ushindi wa madiwani na wabunge nchini kuanzia 1995 hadi sasa. Ikulu ni suala la muda, tena si mrefu”, ameandika Mhe  Joshua Nasari.

Pia Katibu Mkuu wa chama hiko Vicent Mashinji aesema Masha kuondoka CHADEMA ni haki yake kisheria, lakini ni vyema akaweka wazi ukweli wa sababu za yeye kuondoka.

“Mheshimiwa Masha ana haki kisheria, namtakia heri, lakini lazima auambie umma nini hasa kilichotokea”, ameandika Ndugu Mashinji.

Lawrence Masha hapo jana ametangaza kujivua uanachama wa CHADEMA akisema chama hiko hakina malengo ya kushika dola, kama ambavyo malengo ya vyama vya upinzani huwa.

No comments:

Post a Comment

Popular