Waziri mkuu wa Canada Ajibu ombi la Rais Magufuli, asema hawezi kuingilia mahakama. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 15 November 2017

Waziri mkuu wa Canada Ajibu ombi la Rais Magufuli, asema hawezi kuingilia mahakama.

 Ombi la Rais Magufuli, kupitia barua iliyopelekwa na Waziri wa Mambo ya Nje kwenda kwa Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau ili kusaidia kuokoa ndege ya Tanzania iliyoshikiliwa nchini humo limeonekana kukwama

Kwenye barua iliyojibiwa na Waziri Mkuu huyo na kuchapiswa na gazeti la National Post la Canada, Trudeau amesema hawezi kufanya chochote kwa kuwa kesi hiyo ipo mahakamani

'Ni bahati mbaya hali hii imechelewesha ndege hii kutolewa, lakini serikali ya Canada haiwezi kuingilia. Tunaamini mahakama itaamuakwa weledi mkubwa na bila upendeleo'' aliandika Waziri Mkuu Huyo

Ndege hiyo yenye thamani ya dola milioni 32 (sawa na Shilingi bilioni 65) ilikuwa nikati ya ndege tano zilizoagizwa kutoka kwenye kampuni iliyopo Montreal kwa ajili ya shirika la ndege la serikali Air Tanzania

Moja ilikamatwa kutokana na mgogoro na kampuni ya utengenezaji wa barabara ya Stirling Civil Engineering, ambayo inafanya kazi kutoka kituo chake kilichopo Uganda

Serikali ya Tanzania ilivunja mkataba nayo kabla ya kukamilika na kukataa kuwalipa
Stirling, kwa mujibu wa vyombo vya habari ndani ya nchi hiyo. Iliripotiwa kuwa Mahakama ya usuluhishi ilisema kampuni hiyo ilipwe dola milioni 28 kama malipo ya kazi yake pamoja na riba.

No comments:

Post a Comment

Popular