Zitto Kabwe atoboa siri ya tatizo linaloikabili sekta ya madini nchini - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 25 October 2017

Zitto Kabwe atoboa siri ya tatizo linaloikabili sekta ya madini nchini

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe,akihojiwa mubashara na Idhaa ya Kiswahili BBC huko London amesema kuwa mazungumzo na Barrick hayakutatua matatizo ya kudumu kwenye sekta ya madini.

Akihojiwa na Mtangazaji Zuhura Yunus,Zitto amebainisha kuwa matatizo kwenye sekta ya madini ni umiliki na utaratibu kwenye kodi na sheria za kimataifa.

 Zitto amesema lazima swali la nani anamiliki madini lijibiwe ipasavyo. Pia,mfumo wa kodi wa kimataifa unapaswa kuwekwa sawa ili kuzuia ukwepaji kodi, Amesema mambo hayo hayapo kwenye makubaliano na Barrick.

Pia Zitto amesema bila kuangalia vizuri sheria za kimataifa zina sema mini? Atuwezi kufaidika na kitu chochote kile katika sekta ya madini.

Zitto amesema kuwa mafanikio pekee katika mazungumzo hayo ni kufanya mazungumzo na kampuni kubwa kama ya Barrick. Lakini,matatizo yamebaki palepale na vilevile.

No comments:

Post a Comment

Popular