Zanzibar: Rais Dkt Shein atoa maelekezo wizara ya afya - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 25 October 2017

Zanzibar: Rais Dkt Shein atoa maelekezo wizara ya afya

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ameutaka uongozi wa wizara ya afya kuwafamisha wananchi juu ya mikakati ya iliyowekwa na serikali na wizara kwa pamoja juu ya kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wakati katika hospitali zote za Unguja na Pemba.

Agizo hilo alilitoa jana alipokutana na uongozi wa wizara ya afya, ulipowasilisha utekelezaji wake wa mpango kazi wa mwaka 2016/2017 pia kupokea mpango kazi wa Bajeti ya mwaka 2017/2018 na utekelezaji wake kwa kipindi cha robo ya kwanza.

Licha ya bali hiyo alipongeza uongozi wa wizara hiyo kuhusu taarifa ya hali ya upatikanaji wa dawa za maradhi mbalimbali kwa wananchi wa Zanzibar imezidi kuimarika.

"Kuna haja ya kuwajulisha na kuwaelisha wananchi juu ya kuwapo aina mbalimbali za dawa na vigezo vinavyozingatiwa katika utoaji wa dawa hizo ili kuepuka manung'uniko kutoka kwa wananchi", alisema Dkt Shein.

Rais Dkt Shein pia aliwapongeza uongozi na wafanyakazi wote wa wizara ya afya na kuelezea kuna haja kwa wizara hiyo kuendelea kusimamia vema Huduma ya afya kwa wananchi na kuendelea kutoa elimu ya afya kwa jamii.

Pia katika kikao hicho alihudhuria makamu wa pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.

Rais Dkt Shein pia alisifu hatua iliyofikiwa katika kujitolea kutoa damu na kuwpongeza wananchi kwa jinai wanavyojitokeza kwa wingi kutoa damu.

Pia Dkt Shein alitilia mkazo kwa wizara ya afya kutoa mafunzo ya Huduma ya mano kwa kuzingatia kwamba hadi sasa Zanzibar ina wataalam wachache katika fani hiyo.

Rais Dkt Shein alisema itakuwa vema ukiwa chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar ( SUZA) kitaanza kutoa mafunzo hayo pamoja na wizara ya afya kupeleka wanafunzi nje ya nchi kusomea fani hiyo.

No comments:

Post a Comment

Popular