Sauti ya Tundu Lissu yamliza Askofu mkuu wa KKKT - KULUNZI FIKRA

Sunday, 22 October 2017

Sauti ya Tundu Lissu yamliza Askofu mkuu wa KKKT


Askofu mkuu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania ( KKKT) Askofu Frederick Shoo amesimulia alivyobubujikwa na machozi baada ya kusikia sauti ya Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika ( TLS) Mhe Tundu Lissu.

Askofu Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, amesema hayo baada ya jumatano oktoba 18,2017 Baada ya Mhe Tundu Lissu kutoa salaam kwa Mara ya kwanza toka ashambuliwe na watu wasiojulikana, Mhe Tundu Lissu aliwashukuru Watanzania kupitia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na kulunzifikra blog Askofu Shoo amesema alijikuta akitokwa na machozi aliposikia sauti ya Mhe Tundu Lissu kwa Mara ya kwanza toka aliposhambuliwa na watu wasiojulikana na kupelekwa Nairobi kwa matibabu, alisema kupona kwake ni onyo kwa wale wote walio husika na tukio hilo.

"Ninazidi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa jinsi alivyomuokoa na anavyozidi kumpa uponyaji, kupona kwa Tundu Lissu ni jibu la Mwenyezi Mungu na onyo kwa wale wote walio husika na tukio hilo. Mwenyezi Mungu amesema hapana", amesema Askofu Shoo.

Askofu Shoo amesema," Mwenye masikio na asikie, uhai wa mwanadamu ni kitu cha kuheshimu na kila mmoja wetu hata kama uwezo tunao wa kuutoa  ila mwenyezi Mungu hataki na wala hataacha kuwaadhibu yeyote aondoaye uhai wa ndugu yake kwa hiana" amesema Askofu Shoo


No comments:

Post a Comment

Popular