Mbunge wa Iringa mjini ( Chadema) Peter Msigwa ameelezea jinsi anavyosuka mpango wa kumng'oa spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai.
Mhe Peter Msigwa ametangaza nia yake hiyo ya dhati ya kupeleka hoja ya kumuondoa spika Job Ndugai katika mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza mwezi Novemba 7 mwaka huu.
Mhe Peter Msigwa ametangaza hadhima yake hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter alisema amezingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai kwa kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 84 (7) (d) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania", aliandika Mhe Peter Msigwa katika ukurasa wake wa Twitter.
Akizungumza kwa njia ya simu na kulunzifikra blog jana ,Mhe Peter Msigwa ambaye ni miongoni wa wabunge wanaomlalamikia spika Job Ndugai wakidai anaendesha Bunge kwa kwa shinikizo na upendeleo, alisema spika Job Ndugai ameshindwa kuiongoza Tume ya Bunge na Bunge kwa ujumla. "Yeye ni kamishna wa Bunge amekuwa akipokea maelekezo kutoka kwenye mhimili wa utawala ili kuliongoza Bunge. Tume ya Bunge haiendeshwi ipasavyo," alisema Mhe Peter Msigwa.
Mhe Peter Msigwa alimkosoa spika Job Ndugai akidai amekuwa dhaifu katika uendeshaji wa Bunge kuliko maspika wote waliomtangulia na kwamba kipindi chake Bunge limekuwa dhaifu sana mbele ya serikali.
Alipoulizwa kama ataungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge kama ibara ya 87 (7) (d) ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania inavyoelezea katika hoja yake hiyo, Mhe Peter Msigwa alisema hiyo haijalishi ili mradi tu hoja zake hizo ni za msingi na ni za kweli.
"Kupata support hilo ni jambo jingine, tutajenga daraja tutakapofika kwenye mto, kitu cha ni kujenga hoja nzito zinazoelezea kuvunjwa kwa kanuni za Bunge", alisema Mhe Peter Msigwa.
No comments:
Post a Comment