Muigizaji wa filamu bongo Shamsa Ford amemuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, na kumtaka alegeze kidogo kamba ili hali ya maisha ikae sawa kiuchumi.
Kwenye ukurasa wake wa instagram Shamsa ameandika ujumbe akisema hali siku hizi imekuwa ngumu kiasi cha watu kushindwa kufanya yale waliyoyazoea kwenye maisha yao ya kila siku, hata biashara imekuwa ngumu zaidi, na kama kunyooka ilipofikia imetosha.
" Mr President tunaomba ulegeze kidogo hali mbaya baba, tumeshashika adabu sasa hivi na tunaheshimu pesa .Buku sasa hivi tunaiita elfu moja, yaani sijapata hata mialiko ya birthday kubwa kubwa kama ambavyo wanafanyaga.
Mbwembwe hakuna tunaishia kupostiana instagram tu. Baba naomba usikie kilio changu hali mbaya sitaki kurudi iringa kulima mjini patamu jamani. Biashara imekuwa ngumu sana wateja hakuna jamani ...Baba Tuonee huruma jamani tumepauka kweli yaani mpaka ukimuona mwenzio unakimbia", ameandika SHamsa Ford.
Shamsa Ford ambaye kwa sasa ameolewa na mfanya biashara maarufu hapa mjini, amekuwa kimya kwenye sanaa kwa kutotoa kazi mpya kama ambavyo alizoeleka, hali inayozidi kuibua sintofahamu kama inasababishwa na ukata ama la.
Saturday, 21 October 2017
Home
Unlabelled
Bongo movie walionja joto la jiwe wamwangukia Rais Magufuli alegeze kidogo biashara hakuna
Bongo movie walionja joto la jiwe wamwangukia Rais Magufuli alegeze kidogo biashara hakuna
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment