Nchini Malawi kumekua na taarifa za kuwepo kwa watu wanaonyonya damu (vempire) na kuibua hali ya hofu kwa wakazi wa nchi hiyo hasa wanaoishi vijijini, huku kukiwa na vurugu kubwa zinazosababisha mauaji ya watu.
Matukio hayo yaliibuka mwezi Septemba ambapo baadhi ya watu akiwemo mmoja wa wabunge nchini humo, kuthibitisha kuwepo kwa wanyonya damu hao wanaohusishwa na imani za kishirikina, akieleza kwamba watu hao wana vyuma ambavyo watu wakiviangalia hupoteza nguvu.
Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika amewataka wananchi kuacha mara moja vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kuua watu, huku akiwaonya wanyonya damu hao kuacha mara moja matendo hayo ya imani za kishirikina, na atapambana nao akisema vimeisikitisha serikali ya nchi hiyo.
Kufuatia vitendo hivyo watu 8 mpaka sasa wameuawa kwa kupigwa na makundi ya watu, wakiwahusisha na vitendo vya unyonyaji damu, huku mmoja wao akichomolewa kwenye kituo cha polisi alikowekwa na kupigwa mawe na wananchi mpaka kufa.
Nao Umoja wa Mataifa umeondoa baadhi ya wafanyakazi wake kwenye maeneo ambayo yana vurugu zaidi, na kuwaamuru kuhamia sehemu salama zaidi.
Matukio ya vitendo vya unyonyaji damu yaliwahi kuibuka mwaka 2002, huku yakihusishwa na ushirikina kutoka nchi jirani ya Msumbiji.
Saturday, 21 October 2017
Home
Unlabelled
Bara la Afrika lavamiwa na vampire
Bara la Afrika lavamiwa na vampire
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment