Zitto kabwe afunguka sababu ya viongozi wa ACT-WAZALENDO kuhamia CCM - KULUNZI FIKRA

Saturday, 21 October 2017

Zitto kabwe afunguka sababu ya viongozi wa ACT-WAZALENDO kuhamia CCM

Uwepo wa viongozi karibia wote hapa leo unathibitisha tupo imara na tunaendeleza kazi zetu.

Siku chache zilizopita kumekuwa na taarifa baadhi ya viongozi wetu kuondoka na kujiunga na vyama vingine, na pamoja na sababu walizosema kuwaondosha ni pamoja na chama kutofuata misingi iliyoianzisha chama.

Kutokana na maswala hayo nyeti yaliyoelezwa tuliona ni vizuri kuitisha kikao cha uongozi cha kamati ya chama li kujitathimini kujiangalia je ni kweli!

Tangu kuanzishwa kwa chama hiki tumekuwa tukisimamia misingi

Mmoja aliyeondoka kwenye chama tulimuita kwenye kikao hicho ili aje kutusaidia kutufafanulia nakutueleza ni misingi ipi tumeikiuka ili tuweze kiboresha na kusonga mbele. Lakini kwa bahati mbaya hakuweza kufika.

Sisi kama chama cha siasa tunatabua kuwa Kujiunga na chama cha siasa ni hiari hivyo tunawasihi wanachama wetu wanaoondoka waache kuwashawishi wanachama waliobaki.

Wanaodhani ACT Wazalendo ni jukwaa la kusifia chama tawala wajue kuwa si mahali pale. Anasema kiongozi mkuu wa Chama hicho

Hakuna sura ya ukuaji wa uchumi kama serikali inavyodai

Nilimuangalia Prof. Kabudi anaongea hivi nikasema somthing is wrong, aamana anavyokazana kufafanua 50% haiingii akilini

Hakuna jambo jipya hapa ni deal makinga ya serikali.

Tunaambiwa kampuni itahamisha ofisi zake za London na South Africa kuja huku, jamani ofisi ya Acacia ya South Africa teyari ipo Dar es Salaam ndo procument ofice ilikuwa. Ofisi ya London ina watu watano. Tayari sheria ya madini ya mwaka 2010 ilikuwa teyari imeshayasema hayo sio mambo mapya

Sasa watuite vibara watuite wasaliti tutasema tu mpaka wananchi waelewe kwamba haya makubaliano yana matobo

Kabudi ameeleza tu kuwa wanaondoa kodi halafu wanagawanya 50/50, gharama je? Na ndiko ambapo tunapigwa nchi za kiafrika nchi za kimasikini nchi zinazoendelea zinapigwa kwennye mfumo wa kodi wa kimataifa. Kuna kitu kinaitwa base erosion and profit shifting mtatangaziwa huku ni hasara daima ndo maana hatuna faida Wiliamson tulikuwa na 50% Tanzaninte one 25%

Haya ndo mambo serikali haitaki kueleza wananchi ama hawajui au wamekunana mgongoni Bwana turudishie bombadier yetu na sisi tunakuachia huku

Hivi mmejiuliza nini hatima ya ule machanga ulikamatwa bandarini, umerudishwa buzwagi umenasafirishwa mbona hawajasema kwenye yale makubaliano. tuliambiwa kuwa ule mchanga una mamilioni ya hela tuliambiwa kuwa Barrick umehonga watumishi wa umma ndo maana tume na katibu mkuu akafukuzwa sasa mmesikia prosecution yoyote?

No comments:

Post a Comment

Popular