Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imeanza kulima majani aina ya Lusini ambayo ni chakula cha Faru Fausta ili kupunguza gharama za kumtunza mnyama huyo.
Faru Fausta mwenye miaka 54 anahifadhiwa kwenye banda ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ikiwa ni hatua ya kumlinda asiliwe na wanyama wengine kutokana na jicho lake kutoona.
Amekuwa akitumia bandali 250 za majani kila baada ya miezi minne yanayoigharimu mamlaka hiyo Sh5 milioni. Majani hayo hununuliwa kutoka nchi jirani ya Kenya.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Idara ya Malisho na Usimamizi wa Wanyama NCAA, Hillary Mushi amesema mamlaka imeandaa shamba lenye ukubwa wa ekari mbili na imepanda mbegu za Lusini. Amesema ndani ya miezi saba majani hayo yataanza kuvunwa.
Mushi amesema NCAA imechukua hatua hiyo ili kupunguza gharama za kumtunza Faru huyo, ambaye amekuwa moja ya kivutio cha watalii na watafiti kutokana na kuwa ndiye Faru mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani kati ya wanaoishi maeneo ya wazi hifadhini.
"Kilimo cha majani haya kitapunguza gharama za urasimu tuliokuwa tunapata kutoka Kenya, Tumekuwa tukilazimika kupata vibali kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA, mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na Idara nyingine za Serikali. Inatugharimu takriban Sh5 milioni kila tunapoagiza majani", alisema Mushi.

No comments:
Post a Comment