Baadhi ya wabunge wamehoji ni kwanini magari ya wakuu wa mikoa na wilaya yanatangulia mbele huku ya kwao yakiwa ya mwisho katika msafara wa Rais pindi anapotembelea majimbo yao.
Hoja hiyo imeibuliwa leo na Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilal (CCM), wakati akichangia katika semina ya wabunge wa Kamati za Bunge kuhusiana na masuala ya Kidiplomasia na Itifaki.
Naye Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiku (CHADEMA), amehoji ni kwanini wao huwa nyuma huku magari ya wakuu wa mikoa na wilaya yakipeperusha bendera hoja iliyoungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Pareso (CHADEMA) huku Mbunge wa Mtambile Masoud Abdallah (CUF), akiomba apewe ufafanuzi kuhusiana na mambo ya Itifaki.
"Katika ziara hizo gari la Mkuu wa Mkoa huwa inaongoza mbele likiwa na bendera na kufuatiwa na la Mkuu wa Wilaya kisha Mbunge huwa la mwisho, katika hili tunaomba ufafanuzi ni kwanini gari la Mbunge huwa la mwisho katika ziara", amehoji Hilal.
Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Omary Mgumba (CCM), amepingana na wabunge wenzake kwa kudai kuwa Mkuu wa Mkoa na Wilaya wana mamlaka ya kupeperusha bendera kutokana na kuwa Mteule wa Rais ambapo Rais anachaguliwa na watu wa nchi nzima tofauti na Mbunge ambaye anachaguliwa na watu wa jimbo lake tu.
"Mkuu wa Mkoa au Mkuu wa Wilaya anamwakilisha Rais aliyechaguliwa nchi nzima sisi ni vijimbo tu lakini pia wilaya yote ipo chini yake hata kama ni majimbo matano lakini ndiye mwenye kofia mbili kwanza ukuu wa Serikali wa eneo husika na pia ndiye Mwenyekiti wa kamati za Ulinzi na Usalama katika maeneo yao", amesema Mgumba.
Akitolea ufafanuzi jambo hilo, Ofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa, Ally Masabo amesema kiitifaki Mkuu wa Mkoa ndiye anatakiwa kuwa mbele kutokana na kuwa mteule wa Rais.

No comments:
Post a Comment