Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amefunguka kwamba ikiwa wamefanikisha kuupata ushahidi wa rushwa unavyotumika katika ofisi za umma Arusha anauhakika pia wataupata pia ushahidi wa kujua Ben Saanane alipo pamoja na aliyefanya Shambulio la Lissu.
Akizungumza Jana kwenye mkutano alioufanya na wanahabari yeye pamoja Mbungea Joshua na Nassari wa Arumeru Mashariki, wakati walipokuwa wakiuonyesha baadhi ya ushahidi walionao
"Kama ambavyo hili jambo limekuwa 'revealed kwa kiasi hichi huko mbele ya safari tunapoenda mambo ya Ben Saanane yatakuwa wazi pamoja na shambulio la Tundu Lissu. Hivyo tunapeleka ushahidi wote kwa Mkurugenzi wa Takukuru na tunamtaka achukue hatua kama jinsi alivyochukua hatua kwa Rugemalila na wengine" alisema Lema
Aidha Mh. Lema amesema kuwa matukio yanayoendelea ndani ya Mkoa wa Arusha hayawezi kufichika kwa kuwa wao ndiyo wenye mkoa na wanajua namna gani ya kucheza michezo yote hivyo ni vyema watu hao wakachukuliwa hatua ili wasiendelee kukaa ofisini.
Kwa upande wa Mbunge Joshua Nassari amesema kwamba anajua jambo analolifanya linahatari kubwa lakini tayari ameshajitolea hata kufa kwa ajili ya kusema ukweli na kulitetea taifa.
"Nimeondoka Nairobi Lissu bado ni Mgonjwa sana hawezi kufanya lolote. Najua hata sisi ndipo tunapoelekea lakini tumeshajitolea ma tupo tayari. Mimi mke wangu amelia sana leo wakati nikiwa nakuja kuutoa ushahidi huu" alisema Nassari.
Mbali na ushahidi walioutoa Lema pamoja na Nassari wamesema kwamba kwa siku ya leo wametoa sehemu ndogo ya ushahidi wao na kwamba sehemu nyingi watakwenda kuzitoa Takukuru kwani ni aibu na fedheha kutoa ushahidi huo ambao wanaamini utaichafua nchi pamoja na Rais kwa ujumla.
Pamoja na hayo Mh. Lema amesema kwamba pamoja na kwamba ametoa ushahidi huo hadharani hana uhakika kama kuna hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa ingawa ana uhakika na amani kwama ameshatimiza wajibu wake
Sunday, 1 October 2017
Home
Unlabelled
Godbless Lema: Tukio la Tundu Lissu na Ben Saanane mambo kuwa hadharani
Godbless Lema: Tukio la Tundu Lissu na Ben Saanane mambo kuwa hadharani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment