Baraza la wazee chadema watuma ujumbe mazito kwa Rais Magufuli - KULUNZI FIKRA

Sunday, 1 October 2017

Baraza la wazee chadema watuma ujumbe mazito kwa Rais Magufuli

 Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limemwomba Rais John Magufuli kukutana na wazee nchini ili kujadiliana na kupata ufumbuzi wa masuala mbalimbali ikiwepo kupata katiba na miongozo ya kufanya siasa

Wito huo umetolewa leo na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Roderick Lutembeka wakati akizungumza na waandishi wa habari ndani ya makao mkuu ya Chadema jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani.

"Wazee ambao tunashauri Rais Magufuli akutane nao ni wazee kutoka vyama vya siasa, viongozi wastaafu wa dini, wastaafu serikalini na awe tayari kupokea ukosoaji wao na kuufanyia kazi, Mambo mengi yanaendelea ndani ya Taifa letu Rais anapaswa kuyajua na kuyashughulikia" alisema Lutembeka.

Amesema mchakato wa Katiba uliokwama unapaswa kupatiwa ufumbuzi ili kuleta tija kwa Taifa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

"Sisi tunaunga mkonoo chama chetu kudai Katiba mpya. Umuhimu wa Taifa kuwa na Katiba mpya unazidi kuonekana kila siku...Watanzania wanataka Katiba mpya kwa ajili ya kutibu majeraha ya Taifa hili," amesema.

Mbali na hayo Wazee hao wamezungumzia matukio yanayoendelea nchini na kutaja kuwa mengi ni ya kutisha likiwepo tukio la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu, miili ya watu kuokotwa katika fukwe za bahari mauaji na mengine mengi kuwa yanapaswa kufanyiwa kazi.

Aidha Lutembeka amesema wazee wamekuwa hawathaminiwi na kutambulika katika ngazi za uamuzi, afya na ndani ya jamii na kuongeza kuwa sasa ni  wakati kwa Serikali kupeleka muswada wa sheria ya wazee bungeni ili kutekeleza Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003.

No comments:

Post a Comment

Popular