Gari la Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema limechomoka matairi leo Jumatatu baada kudaiwa kuwa limefunguliwa nati 13 kati ya 20 na watu wasiojulikana.
Akizungumza na Mwananchi, Lema amesema walikuwa wamepanga na Mbunge wa Arumeru Mashariki(Chadema), Joshua Nassari kuondoka na gari hilo jana usiku kuelekea Dar es Salaam kuwasilisha ushahidi wa tuhuma za rushwa za madiwani waliohama Chadema.
Hata hivyo amesema majira ya mchana alipokuwa na gari alihisi mlio kwenye tairi ndipo alikwenda kuliegesha hoteli ya Equator.
Amesema kutokana na kulitilia shaka gari aliomba lifti kwenye gari la Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Joseph kwenda naye Dar es Salaam.
"Asubuhi leo (Jumatatu) nikamtuma dereva wangu akachukue gari Equator hoteli alipeleke gereji na baada ya kutoka mita chache tairi zilichomoka," amesema.
Amesema tayari amemuagiza dereva kwenda kutoa taarifa polisi lakini ameiomba kampuni ya ulinzi ya inteligence inayolinda nyumba yake kufanya uchunguzi kubaini watu walioingia ndani na kufungua nati.
"Pia nimeomba wataalam kupitia kamera za nyumbani kwangu kuona kilichotokea kwani kuna uwezekano wa watu kuingia ndani kufanya uhalifu huo.”
Monday, 2 October 2017
Home
Unlabelled
Gari la Lema lachomoka matairi baada ya kufunguliwa nati na watu wasiojulikana
Gari la Lema lachomoka matairi baada ya kufunguliwa nati na watu wasiojulikana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment