Usiku wa kuamkia leo ulikuwa mgumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa.
Nimetumia muda mwingi nikitafakari na kumfikiria sana mwanasiasa mwenzangu, kaka yangu, mbunge mwenzangu na rafiki yangu Tundu Antiphas Lissu.
Siku zote, katika maisha yetu ya kisiasa, hata katika mambo tunayotofautiana na kupingana nimekuwa nikiamini kwa dhati kwamba tofauti hizo haziwezi zikatufanya tukashindwa kuvuka salama kama Nchi, Kama Taifa.
Kilichotokea na kumpata ndugu yetu Lissu jana, ni kitendo cha kihalifu na kisichoendana kabisa na utamaduni wetu wa ustahimilivu na undugu ambao nchi yetu imekuwa ikisimamia.
Kitendo kile cha kikatili kinakwenda kinyume kabisa na misingi ya utaifa wetu ambao tumekuwa tukiujenga kwa miaka 25 sasa kwa kuwa na taifa huru kidemokrasia.
Watanzania tunaolitakia mema taifa hili tuna kila sababu ya kulaani na kukataa kabisa utamaduni huu wa kimafia kuzoeleka katika taifa letu.
Friday, 8 September 2017
Home
Unlabelled
Zitto kabwe: Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ngumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa
Zitto kabwe: Usiku wa kuamkia leo ulikuwa ngumu zaidi kwenye maisha yangu ya kisiasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment