Spika Ndugai: Lissu alishambuliwa kwa risasi 28-32 lakini zilimpata tano - KULUNZI FIKRA

Friday, 8 September 2017

Spika Ndugai: Lissu alishambuliwa kwa risasi 28-32 lakini zilimpata tano

 Kamati ya Uongozi na Tume ya Bunge ilikutana kwa dharura na kukubali kutoa nusu ya posho ya Wabunge ya leo kusaidia matibabu ya Lissu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema Bungeni kuwa gari ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu lilishambuliwa kwa jumla ya risasi 28 hadi 32 lakini zilizompata na kumjeruhi Tundu Lissu ni tano tu.

Spika amesema kuwa, familia ya Lissu ndio walichagua ndugu yao kwenda kutibiwa Nairobi lakini Bunge lilikuwa limejiandaa kumpeleka Muhimbili.

Ndugai amesema kwa hesabu alizofanya kwenye kikao cha Wabunge waliopo leo, kiwango cha mchango wa wabunge kitakua Tshs Milioni Arobaini na tatu (Tsh 43,000,000/=) ambacho ni jumla ya nusu ya posho za wabunge waliohudhuria kikao cha leo.

No comments:

Post a Comment

Popular