Dodoma.Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameeleza alichoambiwana Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu jana Alhamisimchana wakati wakitoka bungeni huku wakicheka.
Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.
”Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini jana wakati Lissu akipelekwa Kenya alisema ameambatana na mkewe, madaktari wawili wasio na mipaka; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Ndege iliyomsafirisha iliondoka katikaUwanja wa Ndege wa Dodoma saa sita na robo usiku.
Friday, 8 September 2017
Home
Unlabelled
Nape aelezea walivyokuwa wakitaniana Jana mchana na Mhe Tundu Lissu.
Nape aelezea walivyokuwa wakitaniana Jana mchana na Mhe Tundu Lissu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
-
Tanzania imechanua na kufanya vizuri katika viwango vilivyotolewa na mfuko wa Mo Ibrahim uliopima hali ya utawala bora na maendeleo na ku...
No comments:
Post a Comment