Nicholas Gyan afunguka mengi, ahidi makubwa kwa mashabiki wa simba sc. - KULUNZI FIKRA

Friday, 8 September 2017

Nicholas Gyan afunguka mengi, ahidi makubwa kwa mashabiki wa simba sc.

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Nicholas Gyan amefunguka kuwa anajua benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha wake, Joseph Omog, linahitaji magoli mengi kwenye msimu huu wa ligi kuu kupitia kwake, hivyo yeye ameshajiandaa kulibeba jukumu ilo kwa kufunga kila atakapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Mghana huyo ambaye ameungana na raia mwenzake, James Kotei, amesajiliwa kwenye kipindi hiki kwa ajili ya kuongezea nguvu safi ya mshambuliaji ya Simba SC, baada ya mabosi wa timu hiyo kuridhishwa na kiwango chake alichokionyesha na moja ya klabu za kwao.

Gyan ameshaitumikia klabu ya Simba SC katika michezo miwili ya kirafiki mmoja wa Simba day dhidi ya Rayon sport ya Rwanda na Hard rock ya Pemba ambapo kwenye mchezo hiyo tayari amefunga goli moja.

Akizungumza na kulunzifikra blog, Straika huyo alisema " Najua watu wa hapa kuanzia viongozi hadi makocha wameweka imani kubwa kwangu kwamba nitawafungia magoli kama ilivyokuwa nafanya nyumbani na kwa sababu hiyo ndiye maana walinisajili na kunileta kuungana na wao msimu huu.

"Kwangu naamini sitashindwa kufanya hivyo kwa sababu nilijipanga zamani kuhakikisha nalifanya hilo na pia ukiangalia suala la kufunga kwangu sio tatizo, tangu natoka nyumbani nimekuwa nafunga na hapa nilipo nitaendelea rekodi yangu ya kufunga", alisema Gyan.

Aidha, Gyan amesema kuwa amelipata begi lake lililokuwa na vifaa vyake vya michezo  limepotea uwanja wa ndege alipowasili Dar es salaam wikieni iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Popular