Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kudai amerudi nchini akiwa na unyenyekevu mkubwa zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri alionyeshwa na Mbunge Tundu Lissu pindi alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.
Zitto ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook asubuhi ya leo na kusema japo Lissu ameumizwa sana lakini hakuacha kumuonyesha ucheshi licha ya kuwa na maumivu makali aliyokuwa nayo katika mwili wake.
"Siku mbili hizi nilizomuona Lissu kitandani zimeniacha nikifikiria sana, nimerudi nchini nikiwa kwenye unyenyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao ndugu yangu amenionyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali. Siyo mara nyingi hapa nchini utasikia tukiongelea ujasiri lakini namfikiria lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi, najua hivyo ndivyo alivyo", ameandika Zitto.
Pamoja na hayo, Zitto ameendelea kwa kusema "waliomshambulia wamemuumiza kweli na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri, alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu siyo kitu rahisi kwa mtu yeyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumie moyo kama asingesema maneno haya kwangu kuwa tumeshinda", amesisitiza Zitto.
Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata, ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.
Monday, 18 September 2017
Home
Unlabelled
Zitto kabwe : Nimerudi na unyenyekevu
Zitto kabwe : Nimerudi na unyenyekevu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment