Omog ahakikishiwa ulaji Simba Sc - KULUNZI FIKRA

Monday, 18 September 2017

Omog ahakikishiwa ulaji Simba Sc

 
 Kamati ya Utendaji ya Simba pamoja na rais wao, Salim Abdallah 'Try Again'  wamemuhakikishia kocha wao mkuu, Mcameroon Joseph Omog kuwa kibarua chake kipo pale pale na aachane na wazushi wanaozungumza pembeni kuwa amepewa mechi tano.

Hivi karibuni kumekuwa na minong'ono kuwa kikosi hicho kina mpango wa kumtimua Omog na amepewa mechi tano kwa sababu hawajaridhika na uutendaji wake wa kazi.

Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara alisema: "Kabla ya mechi na Mwadui, rais wa timu, Salim Abdallah 'Tray Again' alizungumza na Omog alimweleza,Kamati ya Utendaji pamoja na yeye, wanaimani naye, hivyo afanye kazi kwa uhuru, bila shindikizo lolote,  uongozi uko nyuma yake na unamsapoti kwa kila hari,"

"Hakuna taarifa iliyotoka na uongozi wala kwa  mimi Haji kuwa, Omog amepewa mechi tano za uangalizi, hajapewa,   sijampa na hatutampa,"alisema Manara.

Manara amesema, anashangazwa na hilo, na kwamba watu wanaona kama ni desturi ya kubadilisha kocha kila wakati wakati Omog anafanya vizuri.

No comments:

Post a Comment

Popular