Askari anayejiita Faru John ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam alikohojiwa na kuruhusiwa kuondoka akaendelee na kazi.
Kuripoti kwa askari huyo kunatokana na agizo alilolitoa juzi Jumapili, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Peter Sima awe amempeleka leo Jumatatu baada ya kutuhumiwa na wananchi wa Mbagala kwamba amekuwa akidai rushwa.
Kamanda Mambosasa pia ametoa wiki moja kwa Kaimu Kamanda Sima awe amefuatilia tuhuma za rushwa zilizowasilishwa kwake na wananchi.
Amesema askari huyo ataendelea kufuatiliwa ili kubaini ukweli wa tuhuma zilizotolewa dhidi yake na endapo zitathibitishwa taarifa zitawasilishwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro na atachukuliwa hatua za kisheria.
“Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke alimleta huyu askari ambaye nimemuhoji na kumruhusu kuendelea na kazi wakati akiendelea kuchunguzwa ndani ya wiki moja,” amesema Kamanda Mambosasa.
Akizungumza na wakazi wa Mbagala, walilalamika wakidai askari huyo anayejiita Faru John amekuwa akiwakamata wafanyabiashara na kudai kwa nguvu rushwa ya Sh20,000.
Wananchi hao wamelalamika kuwa, mfanyabiashara ambaye hatoi fedha hizo hufungwa pingu na kuzungushwa usiku kucha akiwa kwenye gari la polisi.
Kamanda Mambosasa aliyekuwa akisikiliza kero za wananchi wa Mbagala Zakhem alisema Jeshi la Polisi haliwezi kuwa na askari anayejipa jina la mzaha, huku akiwakandamiza wananchi.
Monday, 18 September 2017
Home
Unlabelled
Askari aliyepachikwa jina ' Faru John' ahojiwa na kamanda Mambosasa
Askari aliyepachikwa jina ' Faru John' ahojiwa na kamanda Mambosasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment