Zitto kabwe: Kupigwa risasi kwa Lissu unahitajika uchunguzi wa kimataifa - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 September 2017

Zitto kabwe: Kupigwa risasi kwa Lissu unahitajika uchunguzi wa kimataifa

Mbunge wa Kigoma mjini na kiongozi mkuu wa  chma ACT-wazalendo, Zitto kabwe amesema unahitajika uchunguzi wa kimataifa dhidi ya shambulio la Mbunge wa Singida mashariki, Tundu Lissu.

Akituma ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter, Zitto kabwe amesema kwamba vyombo vya ndani vinaweza visiaminike kiutokana na uzito wa tukio hilo.

Amesema kwamba " Washambuliaji wa Lissu wamelenga kutunyamazisha. Iwapo tutaendelea kunyamaza watashinda. Hatuwezi kuwapa nafasi hiyo tunaongea kuhusu haki", amesema Zitto kabwe.

Lissu alishambuliwa Alhamisi ya wiki hii wakati walipokuwa akifika nyumbani kwake mjini Dodoma akitokea katika vikao vya Bunge.

No comments:

Post a Comment

Popular