Bavicha kuwashughulikia wasiojulikana kama jeshi la polisi wameshindwa - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 September 2017

Bavicha kuwashughulikia wasiojulikana kama jeshi la polisi wameshindwa

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) wameahidi kushughulika na watu wanaodaiwa wasiojulikana wanaotekeleza matukio ya uhalifu yakiwepo ya uuaji, utekaji, na uchomaji moto ofisi za wanasheria.

Akizungumza na Wanahabari leo kwenye makao makuu ya Chama , Kinondoni jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrobas Katambi amesesema hayo huku akiwataka viongozi wa vijana nchini kuandaa utaratibu wa kuwashughulikia watu hao wasiojulikana.

Aidha, Katambi amesema kuwa vijana wanapaswa kuchukulia jambo la Lissu kupigwa risasi kwa uzito ikiwa ni pamoja na kuonyesha kuchukizwa na mattukio ya kihalifu yaliyowahi kufanywa huko nyuma na watu wanaotajwa kuwa 'wasiojulikana' na kama watashindwa basi atajiuzurru wadhifa wake.

"Natoa agizo kwa viongozi wote wa vijana hapa nchini kuratibu utaratibu mzuri wa chinichini namna ya kuwashughulika hawa wahalifu ambao hawajulikana. Inawezekana hawa watu wasiojulikana wananguvu kuliko vyombo vya dola. Naomba niseme tutawashughulikia kwa namna isiyojulika, kwasababu wao ni watu wasiojulikana. Nitajiudhuru nafasi yangu endapo hili litashindikana.

Pamoja na hayo Bw. Katambi ameongeza kwamba viongozi wa kisiasa wanapaswa kukutana kwa ajili ya majadiliano ya ya matukio yanayotokea kwani hali ya hatari haipo kwa CHADEMA tu bali kwa viongozi wote huku akitolea mfano tukio la viongozi wa CUF walipovamiwa wakiwa kwenye mikutano.

"Napendekeza viongozi wa kisiasa waweze kukutana kwa ajili ya majadiliano ya namna gani ya kukabiliana na hawa watu wasiojulikana wakadhibitiwa. Mfano Alphonce Mawazo, aliyeuawa na watu wasiojulikana, lakini Ben Saanane naye amepotezwa na watu wasiojulikana na hata viongozi wa CUF walivamiwa mkutanoni na watu wasiojulikana. Ni vyema jambo hili mlizingatie sana.

No comments:

Post a Comment

Popular