Chadema Serengeti watoa tamko kulaani shambuliola bunduki kwa Mhe Tundu Lissu - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 September 2017

Chadema Serengeti watoa tamko kulaani shambuliola bunduki kwa Mhe Tundu Lissu

TAMKO LA CHADEMA KANDA YA SERENGETI KULAANI SHAMBULIO LA BUNDUKI KWA MHE TUNDU LISU

1.0 Utangulizi.

Ndugu wanahabari,
Tumewaiteni hapa mtusaidie kuujulisha umma juu ya jambo baya sana linalokabiri taifa letu. Taifa letu la Tanzania limeingiliwa na Mtu asiyejulikana/ watu wasiojulikana wenye nia ya kuvuruga amani na kuleta machafuko. Mtu huyo asiyejulikana amekuwa akiteka, akitesa na kuua watu mashuhuri katika nyanja mbalimbali. Mnamo alhamisi tarehe 07/09/2017 mjini Dodoma. Mtu asiyejulikana alimshambulia kwa risasi takribani 32. Mhe Tundu Lisu (MB) Singida Mashariki, Rais wa TLS na Mwanasheria mkuu wa CHADEMA.

Ndugu wanahabari.
Tukio hili limetushitua sana wanachadema katika kanda ya Serengeti yaani mikoa ya Mara, Shinyanga na Simiyu. Tumeshituka kwani mashambulio ya risasi kwa watu mashuhuri ni dalili ya taifa kuingia katika machafuko. Mataifa yote yaliyoingia machafukoni kwanza hutokea mtu asiyejulikana anaanza kuua watu mashuhuri katika taifa hilo. Mtu asiyejulikana huwa ni nabii wa ghasia na mauaji makubwa kwa taifa, Kwa mara ya kwanza katika taifa letu, awamu hii ya tano maarufu kama awamu ya Magufuli, tofauti na awamu zingine zote tumepata mtu asiyejulikana anayeteka na kuua viongozi wakisiasa na watu mashuhuri katika nyanja mbalimbali.

Ndugu wanahabari.
Historia ya mtu asiyejulikana katika mataifa na jamii mbalimbali ni mbaya sana.

Nchini Rwanda kabla ya mauaji ya halaiki yaliyopoteza uhai wa watu zaidi ya laki nane. Alikuwepo mtu asiyejulikana aliua viongozi mbalimbali.

Mtu asiejulikana alimuua waziri mkuu wa nchi hiyo Bi Agathe Uwilingiyimana tarehe 07/04/1994 hii ilikua kabla ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na mauaji ya halaiki kuanza. Mtu asiyejulikana hakuishia kuua viongozi na watu mashuhuri tu alienda mbali na kulipua ndege ya raisi wa Rwanda wakati huo Bw Juvenal Habyalimana akiwa pamoja na Rais wa Burundi Cyprian Ntaryamira tarehe 6/04/1994.

Baada ya Mtu/watu wasiojulikana kufanya mauaji ya mara kwa mara hatimaye yakalipuka mauaji ya kimbari katika nchi hiyo Rwanda.


Nchini Burundi baada ya mpinzani na mwanademokrasia wa siku nyingi Bw Melchior Ndadaye kushinda urais wa nchi hiyo. Ndani ya miezi mitatu tu ya utawala wake akatokea mtu asiyejulikana nchini humo akiua viongozi na watu mashuhuri, mwishoni mtu huyo asiyejulikana na wenzake akamuua Rais wa Nchi hiyo Bw Ndadaye. Baada ya kifo cha Ndadaye ambaye ndie alikua tumaini la raia wengi Burundi ndipo yakaanza mauaji ya kulipiza kisasi mwisho ikawa vita kamili ya kiraia yaani ‘Civil war’

Nchini Uganda pia aliwahi kutokea mtu asiyejulikana enzi za utawala wanduli Idd Amini, huyu mtu asiyejulikana wa Uganda pia aliua, aliteka na kutesa watu mashuhuri na wanasiasa wenyemlengo unaokizana na wa serikali ya Dikteta Idd Amini. Mtu asiyejulikana wa Uganda aliimuua askofu Janan Jakaliya luwum wa kanisa la Uganda (Anglikana) tarehe 17/02/1977 ambaye alikua mkosoaji mkuu waserikali ya Dikteta Nduli Idd Amini Dada. Mauaji yaliyokuwa yakifanywa na mtu asiyejulikana wa uganda yalipelekea kuongeza chuki kati ya serikali ya Dikteta Amini na raia wa kawaida. Mwisho ilipotokea vita nchini uganda raia waliuungana na upande tofauti na serikali kwa lengo la kuumtoa Dikteta Amini mwenye serikali iliyoibuka watu wasiojulikana.

2.0 Ndugu wanahabari.
Kuibuka Mtu/watu wasiokulikana wa Tanzania ambao wamekuwa wanateka {si kwa kupata fedha} kama walivyomteka mwasiasa kijana wa Chadema bw Ben Saanane ambae hajulikani haliko hadi sasa. Kuuawa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Geita Hayati Alphonce Mawazo. Kutekwa kwa mwanamziki wa kufokafoka maarufu kama Roma Mkatoliki na sasa kushambuliwa kwenye lengo la kuua alikofanyiwa kiongozi wetu Tundu Lissu ni alama tosha ya kuwa mtu asiye julikana kaibuka nchini Tanzania katika Awamu hii ya Utawala.

Hivyo baada ya kujiridhisha ya kuwa mtu asiyejulikana wa sasa ni yule mtu asiyejulikana anayeleta ghasia na kuvunja amani katika jamii. Chadema kanda ya Serengeti kwa pamoja tuanatamka yafuatayo..........

1. Tunalitaka jeshi la polisi lijue kuendelea kutuhadaa kuwa Mhe Tundu Lisu kapigwa risasi na mtu asiyejulikana wakati mitandaoni kuna hadi picha za gari ilotumika kumshambulia Mhe Lisu, Tunaomba waelewe sisi wanachadema hatuwaamini na zaidi tunaona wakifanyacho ni maigizo tu. Tunaamini wanajua mwanzo hadi mwisho ya kinachoendelea.

2. Tunalikumbusha jeshi la polisi na vyombo vyote vya usalama ya kwamba sisi bado tunapenda amani ijapokuwa inaonekana wao wameichoka amani. Na kama silaha zao zinasiku nyingi hazijafanya kazi tunawaomba waende Somalia wakapambane na Alshabab au Syria wakapambane na Islamic state . Waache mara moja kutumia silaha kwa rai wasio na silaha yoyote. Au kama wanapenda kupambana na silaha hapa hapa nchini watupe na sisi silaha afu tupambane wote tukiwa na Silaha.

3. Tunalikumbusha jeshi la polisi, kwa mara zote huku mitaani ikitokea mtu kajeruhiwa wakwanza kutuhumiwa na kushikwa (arrest) huwa ni maadui zake. Hivyo tunashangaa kwa nini hadi sasa maadui na watu wasiopendezwa na harakati za Tundu Lisu hawajashikwa (arrest). Taifa na Dunia nzima inajua mara ngapi Mh Lissu (Mb) amekuwa akishitakiwa, amekuwa akikamatwa na kutishiwa kwa maono ya watu wasiompenda. Tunashangaa leo ameshambuliwa kwa Bunduki ya kivita lakini hamjajishughulisha hata kuwahoji watu hao ambao mara zote wamekuwa wakitafuta kumdhuru.

4. Tunawaomba viongozi wa kidini, wanasiasa wakosoaji wa Serikali na watu mashuhuri wa kada mbalimbali ikiwemo sanaa MSIOGOPE. Tunasema wasiogope kutoa maoni yao juu ya taifa hili hata kama wanahisi maoni hayo hayatawapendeza watu wasiojulikana. Wasiogope kwani Historia inaonyesha watu wanaojifanya hawana upande kisiasa ndiyo huwa waathirika wa mwanzo ghasia zikibuka katika taifa. Historia inaonyesha tusipowapinga na kupambana na hawa watu wasiojulikana mara zote taifa huingia machafukoni. Na wakati wa machafuko waathirika huwa wengi zaidi ya hawa watakaodhuriwa na watu wasiojulika. Hivyo TUSIOGOPE tupambane na mtu asiyejulikana hadi tumushinde.

5. Tunawalaani hao wanajiita au wanaitwa watu wasiojulikana kwa matendo yao ya kutaka kuingiza hofu na ugaidi katika taifa letu. Tunawaombea kwa Mungu wafe mapema tena mwaka huu, wafe vifo vya aibu ikiwezeka waliwe na mbwa au Mbweha.

6. Tunatangaza na kuwaambia hao watu wasiojulikana wakae wakijua wao na kiongozi waopia mtu asiejulikana kamwe watanzania hatutawaoogopa, tutapambana nao kwa kila silaha tukakayoipata, kwa kila mbinu tutakayoipata mpaka kieleweke. Enyi watu msiojulikana jueni mnawasha moto ambao hamutauzima na tunaamini moto ukataowaka utawafutilia mbali watu wasijulikana katika taifa hili takatifu.

7. Kwa makamanda wa CHADEMA popote ulipo sasa ni wakati wa kujipanga kisaikolojia, kiafya na kifizikia. Tujipange katika kuisimamia ile falsafa yetu ya NGUVU YA UMMA. Niwakumbushe tu hawajawahi kutokea watu/ mtu asiyejulikana akashida falsafa yetu ya Nguvu ya umma. Tuamini hakuna kitakacho tusaidia na kutuokoa dhidi ya kuuwawa, kuteswa na uonevu mbalimbali zaidi ya falsafa yetu. Tujikumbushe popote tulipo kuwa si mwenyekiti Mhe Freeman Mbowe, si katibu Mkuu Mhe Dr Vicent Mashinji atatuokoa bali mkombozi wetu ni falsafa yetu NGUVU YA UMMA. Ni wakati wa kujihoji je uko tayari kwa NGUVU YA UMMA na kama ukiona hautoshi Nyamaza milele, ukiona unatosha jiandae kisaikolojia hadi kifizikia.

8. Ndugu watanzania, Chama chetu tunamini katika Nguvu ya Umma. Naomba mkae mkijua tunaamini hivyo na tutaishi hivyo na tuko tayari kufa hivyo. Hatutakubali watu wasiojulikana kutumaliza. Tutatumia falsafa yetu na mbinu zingine kupamabana kuzia tusife hovyo hovyo

MSIOGOPE MAKAMANDA.

Nzemo RP
Katibu wa Kanda- Serengeti.

8/09/2017

No comments:

Post a Comment

Popular