Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)Tundu Lissu, ajitokeze ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio la kupigwa risasi bosi wake.
Kamanda huyo amesema kwamba sababu ya kumtafuta dereva huyo aliyemtaja kwa jina la Adam ni kwa sababu alikuwa pamoja na majeruhi wakati tukio hilo linatokea.
Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini wahusika.
Kamanda Muroto amesema Polisi Mkoani Dodoma wamekamata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)Tundu Lissu.
Kamanda Muroto amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).
"Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda ya risasi yaliyokutwa eneo," amesema kamanda wa Polisi wa Dodoma.
Saturday, 9 September 2017
Home
Unlabelled
Dodoma: Dereva wa Tundu Lissu, Dkt Mashinji watakiwa kuripoti haraka sana
Dodoma: Dereva wa Tundu Lissu, Dkt Mashinji watakiwa kuripoti haraka sana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment