Mkazi wa Chamwino mkoani Morogoro ajinyonga kwa shuka chumbani kwake - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 September 2017

Mkazi wa Chamwino mkoani Morogoro ajinyonga kwa shuka chumbani kwake

 
 Katika hali ya kusikitisha mtu mmoja aliye julikana kwa majina ya Benja Chaula mkazi wa Chamwino Morogoro amejinyonga hadi kufa akiwa ndani ya chumba chake kwa kutumia shuka ambapo chanzo cha kujiua hakikujulikana mara moja huku ndugu zake wakieleza marehemu alikuwa akilalamika kujisikia vibaya kabla ya umauti wake haujamfika.

Akizungumza kwa masikitiko shangazi wa marehemu Tedy Chaula amesema kwa sikumbili kabla ya umauti kumfika shangazi yake amekuwa akisumbuana na nduguzake kuwa anajisikia vibaya na ndipo baada ya hapo wakashangazwa na hatua aliyochukua.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Chamwino Dismas Makangila amesema amestushwa na kupata tarifa za kifo hicho ambacho nichakusikitisha ambapo baada ya kufika katika tukio hilo ametoa tarifa polisi.

Jeshi la Polisi limefika katika tukio hilo nakuchukua mwili wa marehemu kwa mujibu wa sheria huku taratibu za kiuchunguzi kuhusiana na kifo hicho zikiendele.

No comments:

Post a Comment

Popular