Padri Mapunda:Wapinzani sio maadui, Mfalme Suleimani hakujifanya Mungu mtu, Rais Magufuli ajifunze - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 September 2017

Padri Mapunda:Wapinzani sio maadui, Mfalme Suleimani hakujifanya Mungu mtu, Rais Magufuli ajifunze

PADRI Baptiste Mapunda ametaka Rais John Magufuli kutambua kuwa bila majadiliano na viongozi wengine wa vyama vya siasa vya upinzani, hatma ya nchi itakuwa mbaya sana siku zijazo.

Akizungumza katika Kanisa Katoliki Manzese, jimbo kuu la Dar es Salaam, Padri Mapunda alisema Rais Magufuli awe na busara na kufuata mwenendo wa Mfalme Suleimani ambaye katika uongozi wake alikuwa akiomba muongozo kwa Mungu na hakujifanya Mungu mtu.

“Hata Mungu aliwahi kukosolewa na Nabii Musa pale alipotaka kuwaondoa Waisraeli, sembuse binadamu tunaoishi na kufa?" Amehoji Padri Mapunda.

No comments:

Post a Comment

Popular