Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho.
Habari zilizotufikia asubuhi hii ya leo Jumatano September 6, 2017 ni kwamba Viongozi wanne wa Chama cha Wananchi CUF wamefariki dunia baada ya msafara wao kupata ajali maeneo ya Ubenazomozi Mkoa wa Pwani. Ajali iliyohusisha gari aina ya Noah na Lori katika eneo la Ubena barabara ya Morogoro Mkoani Pwani.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati Viongozi hao wakitokea Dodoma kwenye sherehe za kuapishwa kwa Wabunge wapya wa Chama hicho baada ya gari lao kugongana na Lori.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Habari wa CUF Abdul Kambaya Viongozi waliofariki ni kutoka Wilaya ya Muheza, Tanga ambapo miongoni mwao ni Mgombea Udiwani wa Muheza Mjini, aliyefahmika kwa jina moja Uredi.
Aidha, idadi ya majeruhi haijajulikana ila inasadikika kuwa hawazidi 10 na baadhi yao wapo Hospital ya Tumbi huku akisema chanzo cha ajali hiyo ni gari la wafuasi hao kugongana na lori.
Wednesday, 6 September 2017
Home
Unlabelled
Viongozi wanne wa Cuf wamefariki kwenye ajari wakitokea Dodoma
Viongozi wanne wa Cuf wamefariki kwenye ajari wakitokea Dodoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...

No comments:
Post a Comment