Uongozi wa klabu ya Simba sc wataja wachezaji ambao hawapo kwenye mipango ya kocha Omog. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 September 2017

Uongozi wa klabu ya Simba sc wataja wachezaji ambao hawapo kwenye mipango ya kocha Omog.

Uongozi wa klabu ya Simba SC  umewatoa hofu mashabiki wake kwa kutaja wachezaji wenye majeruhi kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya klabu ya Azam FC.

Hadi sasa klabu ya Simba SC  ina wachezaji wawili wenye majeruhi ambao hawapo kwenye hesabu za kocha Joseph Omog.

Mratibu wa timu Abbas Ally amesema ,Zaidi Mohamed ' Nduda' na Shomari Kapombe ndio wachezaji pekee ambao hawapo kwenye mipango ya kocha Joseph Omog, kuelekea mchezo wao dhidi ya Azam FC jumamosi hii.

"Majeruhi tulionao ni walewale tu ambao kimsingi hawapo kakika program ya yetu, Said Mohammed 'Nduda' anaenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu lakini Shomari Kapombe ambaye alipata majeraha katika timu ya Taifa bado ajaanza mazoezi chini ya uangalizi wa daktari" alisema Abbas Ally.

"Kikosi kipo kambini na kila kitu kinaendelea vizuri kama tulivyopanga, tunaendelea na mazoezi kwa kufuata program ya kocha", Alisema Abbas Ally.

No comments:

Post a Comment

Popular