Msichana wa miaka 20 abakwa hadi kufa,madale-Kinondoni - KULUNZI FIKRA

Friday 8 September 2017

Msichana wa miaka 20 abakwa hadi kufa,madale-Kinondoni

 
 Kundi la vijana wasiofahamika wamembaka msichana wa miaka 20 hadi kufa na kisha kumtupa jalalani maeneo ya jirani na nyumbani kwao Madale Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wakisimulia tukuio wazazi wa binti huyo, wamesema kuwa mpaka majira ya saa nne usiku kuamkia leo Septemba 7 alikuwa nyumbani kabla ya kuwasili kwa vijana watatu waliokuja na pikipiki (bodaboda) na kuanza kuzungumza naye kama marafiki kwa takribani saa nzima na baadae binti yake kuaga akitaka kuwasindikiza na hakurudi tena hadi alipopewa taarifa za kifo hicho.

Aidha Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Madale, Gration Mbelwa ameliomba Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kuwaomba wanafamilia pamoja na rafiki za binti huyo kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwakamata watuhumiwa hao.

No comments:

Post a Comment

Popular