Tundu Lissu apigwa risasi Dodoma na hali yake ni mbaya - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 September 2017

Tundu Lissu apigwa risasi Dodoma na hali yake ni mbaya

Mwenyekiti wa chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamis, nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya

Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa chadema na Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika ( TLS) kwa sasa amepelekwa kwenye chumba cha upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dkt Thomas Kashilillah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamegika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wa Dodoma wakitafakari huku wengine wakilia.

Mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengine wamekataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.

Asubuhi, Lissu alihudhulia kikao cha Bunge na aliomba mwongozo kwa Naibu spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na spika wa Bunge, Job Ndugai, kutathimini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na Almasi kuwasilishwa kwa Waziri mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza.

No comments:

Post a Comment

Popular