Kesi ya Malinzi yasogezwa mbele tena - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 September 2017

Kesi ya Malinzi yasogezwa mbele tena

 
 Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake wawili imeahirishwa baada ya hakimu anayesikiliza shauri hilo kuwa na dharura.

Wakili wa Serikali, Faraj Ngokah ameieleza Mahakama ya Hakimu Kisutu leo Alhamis, kuwa  upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na  Hakimu  anayesikiliza shauri hilo, Wilbard Mashauri ana udhuru.

"Washtakiwa wapo Mahakamani, lakini Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri ana dharura, hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili kutajwa" alidai wakili Ngokah.

Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa aliahirisha kesi hiyo September 21 mwaka huu itakapotajwa.

Mbali na Malinzi, washitakiwa wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Nsiande Mwanga.

Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 28, ikiwemo ya utakatishaji fedha.

No comments:

Post a Comment

Popular