Tshabalala: Azam hawatupi presha kabisa. - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 September 2017

Tshabalala: Azam hawatupi presha kabisa.

 Beki wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ amesema hawana presha yoyote kuelekea katika mchezo wao ujao dhidi ya Azam utakaofanyika Jumamosi hii.

Simba ilianza mchezo wake wa kwanza wa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuifunga Ruvu Shooting mabao 7-0 huku Azam yenyewe ikipata ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Ndanda.

 “Tuko kwenye kiwango kizuri kwa sasa hivyo hatuna wasiwasi wa kupata matokeo ya ushindi,”alisema Tshabalala.

Mchezo huo utachezwa Jumamosi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Azam Complex.

No comments:

Post a Comment

Popular