Serikali ya Zanzibar imekanusha kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad kwamba kuna mkakati maalumu unaowahusisha waganga wa kienyeji kutoka Nigeria, Sumbawanga, Pemba na Unguja wenye lengo la kutaka kumuua.
Akiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Wilaya ya Magharibi A, Unguja, Maalim Seif alidai kuwa zinafanyika njama za kutaka kumuua.
Alidai kuwa waganga hao walisafirishwa na meli ya Serikali hadi katikati ya Bahari ya Hindi eneo la Nungwi kisha ilisimama kwa lengo la kufanya kafara ya kutaka kumuua.
“Nasikia wamejazwa kwenye meli ya Mapinduzi II eti wakijidai kuwa wanawatembeza kwenye visiwa mpaka mkondo wa Nungwi, meli ikasimama kwa takriban saa mbili, ndani kuna kamati ya ufundi iliyoundwa na watu kutoka Nigeria, Sumbawanga, Pemba pamoja na Unguja kumbe walikuwa wanafanya mambo yao ya kishirikina,” alisema mwanasiasa huyo.
Alisema watu hao waliletwa kama wajumbe wa kongamano la diaspora lililofanyika Agosti, huku akidai taarifa za kutaka kuuawa na waganga hao alizipata kupitia waganga wenyewe ambao walidai wamepewa kazi ya kuhakikisha wanamwondoa duniani.
Hata hivyo, akijibu tuhuma hizo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais wa Zanzibar, Issa Haji Ussi alisema kauli za kuhusishwa kwa kongamano hilo kutumika kuwakusanya waganga wa kienyeji kwa imani za kishirikina hazina ukweli wowote.
Ussi alisema kwamba kwa sababu taarifa hizo hazina ukweli wananchi wanatakiwa kuzipuuza na kutoziamini.
“Kongamano letu halihusiani kabisa na masuala ya kishirikina kama inavyodaiwa, ila kama huyo aliyesema kutumika kishirikina kama ana ushahidi ni wakati wake sasa kuweka wazi ili jamii itambue sio kusema ovyo,” alisema.
Waziri Ussi alisema kwamba lengo la kutumia meli hiyo kuwatembeza washiriki wa kongamano lilikuwa ni kubadilishana mawazo ya uwekezaji, huku wakikagua mandhari ya Visiwa vya Zanzibar.
Thursday, 7 September 2017
Home
Unlabelled
Serikali yakanusha kutaka kumuua Maalim Seif kwa kutumia waganga wa jadi
Serikali yakanusha kutaka kumuua Maalim Seif kwa kutumia waganga wa jadi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
-
Tanzania imechanua na kufanya vizuri katika viwango vilivyotolewa na mfuko wa Mo Ibrahim uliopima hali ya utawala bora na maendeleo na ku...
No comments:
Post a Comment