Bashe arusha zigo kwa marais wataafu sakata la mikataba ya mibovu ya madini, ataka kinga yao iondolewe. - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 6 September 2017

Bashe arusha zigo kwa marais wataafu sakata la mikataba ya mibovu ya madini, ataka kinga yao iondolewe.

 
 Mbunge wa Nzega mjini kupitia chama cha mapinduzi, Hussein Bashe amewapongeza wajumbe wa kamati zote mbili kwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuja na ripoti yenye picha halisi ndani ya muda mfupi.

Bashe amempongeza Rais kwa kuamua kwa dhati kuamua kufukua matatizo yaliyopo kwenye sekta ya madini. Bashe amesema, ukisikiliza ripoti ya kamati zote mbili pamoja na nia njema ya Rais, inatakiwa kujiuliza, mabadiliko yaliyofanywa na mawaziri, inawezekana viongozi wao wa juu wakawa hawajui? Amedai ni kitu kisichowezekana kabisa.

Bashe amesema imefika wakati kama nchi kuitazama katiba yetu na sheria zetu kwa sababu maamuzi ya namna hii hayawezi kuwa ya waziri mmoja kaamua peke yake. Amesema waziri anashauriwa na mwanasheria, AG lakini bado anafanya maamuzi yaleyale. Bashe amesisitiza lazima kuwepo na force kubwa juu yake na hapo ndio imefika kama nchi kuwa na mjadala, tunahitaji kuwa na immunity kwa viongozi wetu wakubwa wa nchi?.

Amedai anachokifanya Rais Magufuli ni utashi wake wa nafsi tu na amemaliza kwa kuwataka watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli na wabunge wamuunge mkono kwa kupitia upya sheria.

No comments:

Post a Comment

Popular