Rukwa: Ndege yanusurika kugonga bajaji iliyokuwa ikikatisha uwanja wa ndege - KULUNZI FIKRA

Monday, 11 September 2017

Rukwa: Ndege yanusurika kugonga bajaji iliyokuwa ikikatisha uwanja wa ndege

Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu watatu wamenusurika kugongwa na ndege walipokuwa wakisafiri kwa bajaji iliyokuwa ikikatisha uwanja wa ndege wa Sumbawanga mkoani Rukwa ambapo rubani wa ndege hiyo alifanikiwa kuepusha ajali kwa kuipaisha ndege juu upepo wa ndege ukasababisha bajaji hiyo kupinduka na kujeruhi abiria waliokuwemo.

Kukosekana kwa uzio imara katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga kunaweza kusababisha ajali mbaya kutokana na mazoea ya kukatisha katikati ya uwanja wa ndege kwa watembea kwa miguu, baiskeli, pikipiki, magari na hata mabasi madogo ya wanafunzi na abiria kama ambavyo mwishoni mwa wiki imetokea sintofahamu baada ya ndege moja kunusurika kupata ajali ya kugonga Bajaji iliyokuwa ikikatisha uwanja wa ndege hiyo ikitaka kutua.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ilikuwa majira ya saa nne na dakika ishirini asubuhi ndege ilipokuwa ikitaka kutua uwanjani hapo, rubani alibaini kuwepo kwa bajaji na kupaisha ndege lakini upepo mkali uliweza kupindua bajaji ambayo ilisamasoti mara kadhaa na kuwajeruhi waliokuwa ndani.

No comments:

Post a Comment

Popular