Baraza la maaskofu katoliki watoa tamko la kulaani mauaji na shambulio kwa Tundu Lissu - KULUNZI FIKRA

Monday, 11 September 2017

Baraza la maaskofu katoliki watoa tamko la kulaani mauaji na shambulio kwa Tundu Lissu

 
 Sisi Maakofu wa Baraza la maaskofu katoliki Tanzania, Tulipokutana katika mkutano wetu wa kawaida hapa Dar es salaam, tarehe 8-9 septemba 2017, tunapenda kuungana na watanzania wote na watu wenye mapenzi mema kulaani kwa nguvu zetu zote matendo yote ya vurungu, mauaji na uvunjifu wa amani.

Katika Taifa letu sasa tunashuhudia matendo ya mauaji ya watu wasio na hatua kama ulivyo kule Mkuranga, Rufiji na Kibiti, utekwaji wa watu na kuteswa, utekwaji wa watoto, ulipuaji wa ofisi za watu na hivi karibunij shambulio dhidi ya Mbunge Tundu Lissu.

Tunapenda kutamka wazi na kwa nguvu zetu zote kuwa vurugu na mashambulio ya aina yoyote ile yanalifedhehesha Taifa, Matendo haya ni dhambi, ni uharifu na si utamaduni wetu. Tunaomba yakomeshwe Mara moja.

Sisi maaskofu wa Baraza la maaskofu katoliki Tanzania, tunapenda kutoa pole na tunsali kuwaombea waganga wote wa vurugu hizi. Tunawakabidhi kwa mwenyezi Mungu wale wote waliopoteza maisha yao, ili mwenyezi Mungu awarehemu. Tunawaombea majeruhi wote wapate kupona haraka. Tunatamani kuona wale wote walio nyuma ya matukio haya ya vurungu, utekaji na utesaji wanatafutwa na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Tunaliombea Taifa letu amani na utulivu, tunu ambazo ni matunda ya haki, Uhuru na kujiheshimu.

No comments:

Post a Comment

Popular