Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amefunguka na kudai atahakikisha yeye na wabunge wanampa ushirikiano Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma aliyeapishwa leo baada ya kuteuliwa siku ya jana Septemba 10 mwaka huu.
Ndugai ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anatoa salamu za wabunge katika ghafla hiyo ya uapisho iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa bila ya kumsahau Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
"Sisi kama bunge tunawahakikishia ushirikiano mkubwa sana kwa kuhakikisha kazi za Mahakama zinaendelea kama zilivyo kikatiba na tutaheshimu sana. Yale maneno na makombora moja moja ya bungeni ni vitu vya kawaida, ndiyo utamaduni wa bunge",amesema Ndugai.
Aidha, Ndugai amesema Mahakama inamchango mkubwa kwa wananchi pamoja na taifa kwa ujumla kwa kuwa hicho ndicho chombo pekee kinachoweza kumtetea mnyonge kuweza kupata haki yake kutoka kwa waporaji.
"Kuwepo kwa Mahakama ndiyo usalama wetu, amani, kheri na matumaini ya mnyonge katika sheria na maamuzi ya Mahakama. Kwa hiyo tunakutakia kila la kheri katika kazi yako, tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu na tutakusaidia na kuomba msaada wako",amesisitiza Ndugai.
Kwa upande mwingine, Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma ameahidi kufanya kazi katika maadili ya kisheria pamoja na kurudisha imani ya wananchi kuhusiana na kupata misaada ya kisheria inayotolewa katika Mahakama mbalimbali ndani ya Tanzania.
Monday, 11 September 2017
Home
Unlabelled
Ndugai: Makombola ndiyo utamaduni wetu
Ndugai: Makombola ndiyo utamaduni wetu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment