Mayanja zaidi kuililia safu ya ushambuliaji - KULUNZI FIKRA

Monday, 11 September 2017

Mayanja zaidi kuililia safu ya ushambuliaji

Simba imerejea mazoezini leo kuiwinda Mwadui watakayokutana nayo Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, huku kocha msaidizi wa kikosi hicho, Jackson Mayanja akilia na safu ya ushambuliaji.

Timu hiyo ilitoka sare na Azam katika mchezo wa Jumamosi na jana kocha Joseph Omog aliwapa mapumziko wachezaji wake na leo wamerejea tena mazoezini kujiandaa na mchezo ujao.

Mazoezi hayo pia yamehudhuriwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi na  beki Juuko Murshid ambao hawakucheza mchezo dhidi ya Azam kutokana na kuchelewa kujiunga na timu wakitokea kwenye majukumu ya timu yao ya Taifa ya Uganda Cranes.

Kukosekana kwa Okwi kulionekana kuwachanganya mashabiki wa Simba ambao wameweka imani kubwa kwa mchezjai huyo na kuamini kuwa  uwepo wa mchezaji huyo kikosini  unakuwa mwiba kwa timu pinzani.



 Mayanja alisema bado wataendelea kukazania suala la umaliziaji kwa washambuliaji wake ili kuhakikisha timu hiyo inafunga mabao kila mechi.

"Kila mara tumeona maendeleo katika safu ya ushambuliaji ingawa bado kuna tatizo hivyo tutaendelea  kulifanyia kazi tatizo la ufungaji ili kuhakikisha mechi zijazo timu inafunga na kupata ushindi.

 "Licha ya kwamba kazi ya kufunga ni ya washambuliaji lakini hatutajikita kwao pekee bali kwa wachezaji wote kuhakikisha wanafunga wakipata nafasi. Tunataka tukomeshe tatizo la kukosa mabao na kuhakikisha kila nafasi inayopatikana inatumika ipasavyo ili timu ipate ushindi," alisema Mayanja.

No comments:

Post a Comment

Popular