Rais Magufuli awatumbua viongozi wote waliotuhumiwa na kamati ya madini - KULUNZI FIKRA

Thursday, 7 September 2017

Rais Magufuli awatumbua viongozi wote waliotuhumiwa na kamati ya madini

Rais Magufuli amewataka viongozi mbalimbali wa serikali ambao wametajwa kwenye ripoti za bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite wamepishe nafasi zao ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri kuwachunguza.

Viongozi ambao Rais Magufuli amewataka kuachia nafasi zao ili kupisha uchunguzi wa a tuhuma zinazo wakabili ni Waziri wa TAMISEMI,Simbachawene, Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Edwin Ngonyani na RAS wa Mkoa wa Manyara, Eliakim Maswi.


Rais Magufuli amesema hayo leo wakati akikabidhiwa ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kusema amesikia baadhi ya viongozi mbalimbali wengine ambao amewateuwa yeye kuwa wameusishwa kwenye wizi huo hivyo amewataka wapishe.

"Wako watu wametajwa tajwa, na wengine mimi ndio nilihusika kuwateua sasa ukishatajwa tajwa, naagiza vyombo vya ulinzi na usalama vifuatilie hili tena kwa haraka, Wale ambao wametajwa tajwa kwenye ripoti hii ambao ni wateule wangu, ili vyombo vya usalama viweze kufanya kazi yake vizuri, ni matumaini yangu watakaa pembeni" alisema Rais Magufuli

"Nitashangaa sana endapo watu waliotajwa hawataaanza kukamatwa hata iwe leo wakamatwe tu" alisisitiza Rais Magufuli

Katika ripoti hiyo ambayo iliwasilishwa jana mjini Dodoma na leo kukabidhiwa kwa Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa iliweza kuwataja baadhi ya viongozi wa serikali ikiwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. George Simbachawene, Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na viongozi wengine mbalimbali ambao Rais ameagiza washughulikiwe haraka.

Hata hivyo Rais Magufuli amesema Prof. Abdulkadir Mruma ambaye pia ametajwa katika ripoti hizo alipandikizwa kwa maadui ili kuibua taarifa ya namna nchi inavyoibiwa madini.

No comments:

Post a Comment

Popular