Arusha: Mtekaji wa watoto afariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu kuwatoroka polisi. - KULUNZI FIKRA

Thursday 7 September 2017

Arusha: Mtekaji wa watoto afariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu kuwatoroka polisi.

 Mtuhumiwa Samson Petro ambaye ndie mtekaji na muuji wa watoto wawili Maureen na Ikram amefariki dunia kwa kupigwa na risasi wakati akitaka kutoroka mikononi mwa Polisi jijini Arusha.

Mtuhumiwa alipigwa risasi mbili za miguu wakati akijaribu kutoroka na ndipo alipofariki dunia akiwa hospital ya Mount Meru.

Hapo awali Usiku wa tarehe 2 Septemba kijana mwenye umri wa miaka 18, Samson Petro alishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuteka watoto katika mkoa wa Arusha na Geita.

Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alithibitisha taarifa hizo za kukamatwa kwa mtekaji huyo.

Mwabulambo alisema kuwa kijana huyo alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Shitungului iliyopo mji mdogo wa Katoro akiwa na mtoto mdogo nmwenye miaka miwili.

Alisema mtuhumiwa alimficha mtoto huyo katika chumba namba 11 cha kulala wageni iitwayo Shitungulu wakati akisubiri mpango wake wa kutaka alipwe shilingi milioni nne na wazazi wa mtoto huyo Omben Mshana na Elizabeth Ombeni.

No comments:

Post a Comment

Popular