Watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni wanachama wa Chadema wanashikiliwa na Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa kuhojiwa kuhusu mpango wa maombezi uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Tip -Sinza, wilayani Ubungo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne aliyekuwa uwanjani hapo na kikosi cha askari zaidi ya 25 amesema watu hao walikamatwa saa 3:40 asubuhi wakiwa eneo hilo.
"Tunawashikilia na tutawahoji kama wana uhusiano na kile kilichopangwa kufanyika hapa kwa sababu kilishapigwa marufuku. Kama hawana uhusiano tutawaachia," amesema Kamanda Jumanne.
Amesema, “Atakayetaka kujaribu aje ila cha moto atakiona kwa sababu jitihada za kuzuia watu wema wasikanyage hapa zimeshafanyika sasa wanakuja kufuata nini."
Katika eneo hilo, polisi walikuwa wakiziondoa bajaji wakiwataka madereva wasiziegeshe hapo kwa siku ya leo.
Baadhi ya polisi wameonekana wakiwa na mabomu ya kutoa machozi na walifika uwanjani hapo wakiwa kwenye magari aina ya Toyota Land Cruiser.
Uwanjani hapo hivi sasa ni kweupe kukiwa hakuna maandalizi yoyote kuonyesha kuwa patakuwa na maombezi.
Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo –Chadema (Bavicha) jana Jumamosi lilitoa taarifa likisema leo litaungana na viongozi wa kiroho kufanya maombi maalumu kumwombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayeendelea na matibabu Nairobi, Kenya baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7.
Viongozi wa Bavicha waliofika uwanjani hapo muda si mrefu wamekimbia baada ya polisi kuwafuata walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari.
Sunday, 17 September 2017
Home
Unlabelled
Polisi wafanya doria Sinza kuzuia Maombezi ya Tundu Lissu
Polisi wafanya doria Sinza kuzuia Maombezi ya Tundu Lissu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment