Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee ataongoza mazishi ya aliyekuwa diwani wa viti maalumu Mbeya Mjini, Ester Mpwiniza yatakayofanyika kesho.
Taarifa ya Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Obadia Mwaipalu imesema diwani huyo Ijumaa jioni alianguka nyumbani kwake na alipelekewa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya alikofariki dunia kutokana na shinikizo la damu.
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema Mpwiniza aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bawacha Wilaya ya Mbeya Mjini, alikuwa kiunganishi ndani na nje ya chama hicho, hivyo wameamua kumzika kesho Jumatatu.
Amesema uamuzi huo unalenga kutoa nafasi kwa wageni kuhudhuria maziko wakiongozwa na viongozi wa kitaifa watakaoingia Mbeya leo Jumapili.
“Mama Mpwiniza alikuwa kiongozi mkubwa ndani na nje ya chama, hivyo hatuwezi kuharakisha maziko yake. Tunasubiri viongozi wa kitaifa akiwamo Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Halima Mdee na viongozi wengine. Sijajua makaburi atakakopumzishwa lakini itakuwa ni hapahapa Mbeya Mjini,” amesema Sugu.
Amesema awali walipanga shughuli zote za msiba huo zifanyike Mtaa wa Ghana kwa ndugu wa marehemu lakini baadaye familia ilihamishia kwenye nyumba yake aliyokuwa akiijenga eneo la Iyela jijini hapa.
Mwenyekiti wa Chadema, Mbeya Mjini Mwaipalu amesema, pia wanasubiri utaratibu wa ndugu za marehemu ukamilike.
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mchungaji Peter Msigwa ametuma rambirambi kwa familia ya marehemu, ofisi ya Meya wa Jiji la Mbeya, Chadema na wananchi kwa jumla.
Sunday, 17 September 2017
Home
Unlabelled
Mdee kuongoza mazishi ya diwani wa Chadema
Mdee kuongoza mazishi ya diwani wa Chadema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment