Polisi na mahabusu wapata ajali Mwanza - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 September 2017

Polisi na mahabusu wapata ajali Mwanza

 Gari la polisi lililokuwa limebeba mahabusu jana lilipata ajali eneo la kenyata jijini mwanza kwenye mzunguko wa samaki na kusababisha mahabusu mmoja na askari kupata majeraha.

Gari hilo lenye namba za usajili PT 3643 aina toyota land cruiser pick up lililokuwa limetoka mahakama ya wilaya ya Nyamagana likuwa limewabeba mahabusu wanaodaiwa kuwa ni hatari waliokuwa wanarudishwa gereza la butimba na ghafla lilipofika eneo la mzunguko wa samaki gari namba T 230 BMP aina ya toyota vitz lililookuwa linaendeshwa na happyness clorence ambapo aliliweza kuingia ghafla barabarani na kupelekea ajali hiyo kutokea.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani mwanza naibu kamishna ahmed msangi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema majeruhi wamepatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa mwanza Sekou Toure na kuweza kuruhusiwa.

"Madereva wengi wana dharau na ndiyo maana ajali kama hizi huwa zinatokea. kwa hili lilotokea lingeweza kusababisha matatizo makubwa mno kwani askari wetu walikuwa wapo na silaha nzito na mahabusu waliokuwa wakisindikizwa walikuwa hatari kwani wangeweza kuumia au kupata fursa za kukimbia na ukizingatia askari walikuwa na silaha yangetokea mengine makubwa" Ahmed Msangi.

No comments:

Post a Comment

Popular