Kocha Simba asema amejipanga vyema dhidi ya Azam FC - KULUNZI FIKRA

Saturday, 9 September 2017

Kocha Simba asema amejipanga vyema dhidi ya Azam FC

 
 Benchi la ufundi la Simba chini ya kocha wake mkuu, Joseph Omog, raia wa Cameroon, limeweka bayana kuwa licha ya mchezo wao dhidi ya Azam FC kuhamishiwa katika Uwanja wa Azam Complex ambao unamilikiwa na wapinzani wao hao, lakini suala hilo halitaondoa dhamira yao ya kupata matokeo mazuri ambayo wanayataka.

Simba, leo Jumamosi kwa mara ya kwanza watacheza na Azam katika mechi ya Ligi Kuu Bara ndani ya Uwanja wa Azam Complex baada ya mchezo huo kuhamishwa kutoka Uwanja wa Uhuru, uliopangwa awali kabla ya mabadiliko ya ratiba.

 Mcameroon huyo amesema kuwa hawana wasiwasi kwenda kucheza Azam Complex kutokana na yeye kuujua uwanja huo kutokana na uzoefu wake wa kufanya kazi katika soka la kisasa.

“Hakuna hofu yoyote ya kucheza kwenye uwanja wa wapinzani wetu, kwa sababu tumejipanga kupata pointi na tuna wachezaji wanaoweza kulitimiza hilo, lakini kwenye soka hili la kisasa haijalishi ni wapi ambapo utakuwa unacheza kama umejiandaa vya kutosha wewe ndiye utaibuka na pointi,” alisema Mcameroon huyo.

No comments:

Post a Comment

Popular