Nape Nnauye: Gari lililotumika kumshambulia Lissu limewahi kuripotiwa kuwa linawafuatilia baadhi ya wabunge - KULUNZI FIKRA

Friday 8 September 2017

Nape Nnauye: Gari lililotumika kumshambulia Lissu limewahi kuripotiwa kuwa linawafuatilia baadhi ya wabunge





                                      Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni na kusema;.
"Mimi hili nalisema hadharani. Hii gari imekuwa ikifuatilia baadhi ya Wabunge hapa, mimi nikiwa mmoja wapo. Tulienda tukaripoti kwamba jamani kuna gari inatufuatiliana hatuelewi ni gari ya nani.

Sasa gari hiyo hiyo, namba hizo hizo, idadi ya watu hao hao, halafu watu wanaripoti hatua hazichukuliwi mpaka mwenzetu anafikia hatua ya kupigwa risasi, mimi nadhani ni jambo kubwa.

Ndo maana nikasema, yeye lisu ambaye Maswahiba yamemfika, sisi wengine tuliambiwa wanatufuatilia na tukathibitisha kwamba kweli wanatufuatilia, lakini yeye yamempata kabisa!..kwa kushambuliwa. Nadhani yeye anaweza kutueleza mengi kabisa. Nina hakika Lissu, dereva wake, wana mengi ya kusimulia juu ya hili.

Kwa kuwa alililalamikia kwa muda mrefu basi nadhani ni vizuri yeye aje atueleze. Ukiacha vyombo vya usalama kuchukua hatua lakini na yeye aje atuambie experience, naamini yale aliyoyasema wakati wa nanii yake na wandishi wa habari hakuyasema yote, aje aseme na mengine ambayo hakuyasema". Ameongeza Nape.

Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.

”Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nape Nnauye jana kabla ya Tundu Lissu kupigwa risasi majira ya saa 7 mchana anadai alikutana naye na kuongea naye katika viwanja vya bunge na baadaye kuja kupata taarifa kuwa amepigwa risasi na watu wasiojulikana.

"Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa 'the T460CQV' uliyoilalamikia"aliandika Nape Nnauye kweye mitandao yake ya jamii.

Mpaka sasa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia majeraha ambayo ameyapata katika mwili wake

No comments:

Post a Comment

Popular