Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe amefunguka na kuelezea hali ya Mbunge wa Singida Mashariki na kusema mbunge huyo ameumizwa vibaya na kuwa hali yake toka saa nne za asubuhi leo haikuwa vizuri kutokana na majeraha aliyopata.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiongea na waandishi wa habari nchini Kenya.
Mbowe amesema kuwa Mbunge huyo mpaka sasa bado yupo kwenye chumba cha upasuaji katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea kupatiwa matibabu kufuatia kiongozi huyo kupigwa risasi jana na watu wasiofahamika akiwa mjini Dodoma.
Aidha Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa ambaye naye yupo nchini Kenya amelezea hali ilivyokuwa toka walipofika jana usiku nchini Kenya mpaka dakika za mwisho Mbunge huyo alipoingia kwenye chumba cha upasuaji.
"Mh Tundu Lisu aliwasili usiku majira ya saa saba hapa Nairobi Jomo Kenyatta International Airport na alipokelewa na team ya Madaktari wa Nairobi hospital pale Aairport na matibabu yalianza mara moja kuanzia ndani ya Ambulance hadi hospital. Aidha alipofika Nairobi hospital alifanyiwa vipimo vyote na baadae saa nne asubuhi aliingizwa chumba cha upasuaji" aliandika Peter Msigwa kwenye ukurasa wake wa facebook
Mchungaji Msingwa aliendelea kusema kuwa " Tangu jana alipofika alifanyiwa stabilization ili aweze kukabiliana na surgery na zoezi hilo lilifanikiwa vizuri na madaktari wametueleza kuwa hakuna hali yoyote ya hatari na matibabu yake yanaendelea kwa mafanikio hadi sasa majira ya saa 9 alasiri bado hajatoka theatre na madaktari wametueleza kuwa wanaendelea vizuri"
Friday, 8 September 2017
Home
Unlabelled
Mbowe azungumzia hali ya Tundu Lissu
Mbowe azungumzia hali ya Tundu Lissu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment