Mwambeleko aongeza ushindani wa namba kwenye klabu ya Simba SC - KULUNZI FIKRA

Friday, 8 September 2017

Mwambeleko aongeza ushindani wa namba kwenye klabu ya Simba SC

Kiraka wa Simba, Jamal Mwambeleko ameweka wazi asili ya nafasi anayocheza uwanjani ni winga ya kushoto yaani namba 11 na siyo beki wa kushoto kama alivyozoeleka.

Mwambeleko ambaye amesajiliwa na Simba akitokea Mbao FC ya Mwanza, wadau wengi wa soka wamezoea kumwona akicheza beki ya kushoto na wanaamini ndiyo nafasi yake ya kudumu.

Lakini, mchezaji huyo amefafanua, klabu ya Mbao ndiyo iliyosababisha akajulikana kwa namba hiyo: "Wakati nacheza Mbao, ikatokea shida kwenye nafasi ya beki wa kushoto wote walikuwa wanaumwa, ndipo kocha aliamua kunibadilisha nikawa nacheza huko."

"Lakini, hapo awali nafasi niliyokuwa nacheza ni winga na ndiyo nakuwa huru ninapocheza. Isipokuwa katika mimi ni mchezaji hivyo, sitakiwi kuchagua namba, popote ninapopewa majukumu na kocha unafanya kazi," alisema Mwambeleko.

Hata hivyo, kutua kwake Simba kutokana na mfumo ambao unatumika, amekutana na ushindani  kwani nafasi hizo kuna wachezaji kama, Jamal Mnyate, Mwinyi Kazimoto, Mohamed Ibrahim 'Mo'na Emmanuel Okwi raia wa Uganda. Kwenye beki ya kushoto kuna Erasto Nyoni na Shomari Kapombe ambaye kwa sasa ni majeruhi.

No comments:

Post a Comment

Popular